CUF HAIHUSIKI NA NJAMA ZOZOTE DHIDI YA CHADEMA KWENYE SAKATA LA ZZK;
Wadau,
waandishi wengi wa habari wananipigia nithibitishe ikiwa CUF iliandaa
makundi ya wanachama wakamshabikie ZZK mahakamani leo hii. Taarifa ya
namna hii pia imeenea mitandaoni.
Pia
viongozi kadhaa wa CHADEMA wamenipigia kunijulisha kuwa Intelijensia
yao imegundua kuwa vijana wa CUF wamepenyezwa na kwamba wamevushwa
T-SHIRT za M4C na mapanga.
Napenda
kuwajulisha wadau wote kuwa CUF haijapanga wala kutuma makundi ya
vijana kwenda kumshabikia ZZK. Ikiwa pana wanachama wa CUF wameonekana
mahakamani itakuwa wamekwenda kwa Utashi na Matakwa yao.
Sisi
chama Taifa hatujawahi kukutana, kupanga wala kutuma vijana wa CUF
wakasimamie upande wowote katika mgogoro huu. Wakati wa fukuto la HAMAD
RASHID na CUF watu wengi tu raia walifika mahakamani, sie hatukuwa
kuhoji na kutafuta vyama vyao, tuliamini ni watanzania tu.
Ni
ushauri wangu kuwa, panapokuwa na kesi inayovuta hisia za watu
haitajalisha watu hao wanatoka makundi gani, mwenye kutaka kwenda
atakwenda tu.
Ni
vigumu kwa chama chetu kukataza wanachama wake wasihudhurie kesi ya
Babu Seya, ya Sheikh Ponda, ya Zitto Kabwe, ya Samaki wa magufuli n.k.,
Unapokuwa na chama chenye mamia elfu ya wafuasi si rahisi kujua mfuasi
yupi yuko wapi kwa wakati gani anafanya nini na ametumwa na nani.
Lakini
kwa ajili ya kujenga mshikamano wa vyama vyetu, tunachunguza taarifa
hizo ili kubaini kama ni kweli palikuwa na wanachama wetu mahakamani na
tukiwabaini tutawahoji na kujua nani aliyewatuma na tutaona hatua za
kuchukua.
Ikumbukwe
kuwa mwenyekiti wa chama chetu taifa Prof. Lipumba wakati akisoma
maazimio ya kikao Cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa mwezi Desemba mwaka
jana alieleza kuwa Baraza Kuu la CUF linawaomba CHADEMA wamalize
mgogoro wao haraka ili tuwekeze nguvu za upinzani katika kuunganisha
umma kutafuta katiba ya watanzania katika bunge la katiba, Msimamo wa
CUF ni kutokuwa na upande katika mgogoro huu.
Tunatoa
wito kwa viongozi wa CHADEMA kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na
usalama iwapo wataona au kuhisi kuna mwananchi au mfuasi wa chama chetu
amejiingiza katika mgogoro wao na kwamba amehatarisha amani ili sheria
ichukue mkondo wake.
CUF
itaendelea kuiheshimu CHADEMA kama taasisi inayojitegemea. Hatukuwahi
kuingilia, kushabikia wala kupinga masuala na maamuzi ya ndani ya
CHADEMA, tukiona pana jambo linatugusa mara zote huwa tunatoa ushauri
wetu tu na sio kuingilia masuala ya ndani ya vyama vingine.
______________________________ __
Julius Mtatiro,
National Deputy Secretary General,
The Civic United Front(CUF),
Tanzania Mainland,
P.O Box 10979,
Dar Es Salaam.
Phone; +255717536759,
Email; juliusmtatiro@yahoo.com
Twitter; https://twitter.com/Julius_ Mtatiro
No comments:
Post a Comment